Familia za watu waliouawa Takriban watu 20 wameuawa na wengine kujeruhwia kwenye madhababu yaliyo mji wa Sargoda, mkoa wa Punjab nchini Pakistan.
Naibu kamishna wa polisi Liaquat Ali Chatta, alisema kuwa mshukiwa mkuu ni mhudumu wa madhabu hayo Abdul Waheed.
Manusura mmoja aliwaambia polisi kuwa bwana Waheed aliwaita wafuasi katika chumba chake mmoja baada ya mwingine, na kuwapa chakula kilichokuwa na sumu.
Yeye na wenzake kisha waliwaua watu hao kwa kuwapiga wakitumia vifaa.
Kisa hicho kilifichuliwa na mwanamke aliyekuwa amejeruhiwa katika hospitali iliyo karibu, ambaye alikuwa amefanikiwa kutoroka.
Mwana wa Osama bin Laden asakwa na Marekani
Iran yawanyonga ‘magaidi’ 20
Mashambulio Kashmir: India yadai kulipiza kisasi
Kisha polisi walifululiza kuenda eneo hilo na kumkamta bwana Waheed pamoja na watu wengine ambao wanaaminiwa kuwa washirika wake.
Sababu ya mauaji hayo haijulikani lakini polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo alionekana kuwa na matatizo ya kiakili.
Abdula Waheed mweye umri wa miaka 50, amekiri kuwaua watu hao, kwa sababu alihofu kuwa walikuwa wameenda kumuua, kwa mujibu wa AFP