SIMULIZI >USIMUAMINI

Bora tu kuwa muwazi nakupinga uongo wakumpamba kwa maneno mazuri yanayomfanya umuone mwema!

fungu utakaloniweka utajua mwenyewe ila mimi nakuambia ukweli USIMUAMINI! ndio, usimuamini kwa lolote asemalo labda akuthibitishie kwa vitendo nawewe ujiridhishe kweli ametenda yeye maana uongo upo hata kwenye utendaji!

tangu kuzaliwa kwake jicho hili limeona mengi nakujifunza vingi pia, moja ya fundisho ndilo hilo nakuasa nalo KAMWE USIMUAMINI!

nimuongo, mzandiki na mjanja kupindukia ukiyaamini majibu yake hakika utapotea, suala la msingi ni moja tu usimuamini!

kama huniamini hebu Tafuta vitabu vyooote vya mapenzi na usome hulka za wapendanao nina uhakika hakuna hata mmoja aliyewahi jibu kuwa sio muaminifu pindi alipoulizwa na mwanza wake kama ni muaminifu!

uhakika ninao kila mmoja hujibu kuwa yeye ni muaminifu tena wa kiwango cha juu tena ubaya zaidi huweza hata kupitisha kidole chake shingoni akiapa kwa jina la MUNGU wake kuwa yeye ni muaminifu wakati ukweli sio huo! hata HOFU ya MUNGU hana aisee USIMUAMINI!

ukiutafuta ukweli unaweza kubaini kuwa yeye ni bingwa wakudanganya, moyo wake umezingirwa na wapenzi lukuki, na kila mmoja amempa nafasi kubwa yakuutalii mwili wake! Yani sijui hata kwanini siku hizi uongo ndio pambio la mapenzi nina uhakika kama ingekuwa sio hivyo walau asingeongopa kuwa yeye ni muaminifu wakati ni zaidi ya mzinifu, bingwa wakucheza mechi za nje!

usimuamini sababu hakuna aliye mkweli katika mahusiano nionavyo mimi kila mmoja sasa hivi ana tamaa ya kile anachokikosa kwa mpenzi wake.

usimuamini kabisa maana ukitafuta kote ulimwenguni utagundua kuwa ni wachache mno waliopata ujasiri wakujitangaza kuwa wameathirika na UKIMWI, wengi wanavinjari nawadudu huku wakionesha ubukheri wa afya kumbe ukweli damu zao ni HATARI TUPU na ibilisi wa roho mbaya anawaongoza kusambaza bila huruma, pengine uliye nae sio mmoja wao lkn unajuaje kama amekutana na watu wa aina hii akawaamini nakujizolea maradhi! tafadhali ndugu yangu USIMUAMINI maana hata yeye pengine hajijui.

kutokumuamini mtu sio dhambi wala jinai nijuavyo mimi ni njia nzuri ya kujihami na maovu, majuto pamoja na athari nyengine zitokanazo na walimwengu walioficha mengi mioyoni mwao.

Usimuamini kabisa maana hata wewe sidhani kama ulishawahi kusema kwa mpenzi wako kuwa ulimsaliti au unamsaliti na rafiki yake au mtu yoyote wa nje, nijuavyo mie ni lazima unampamba kwa maneno mazuri ya uongo ukijinasibu kuwa wewe ni mtulivu, muaminifu na kamwe hutakuja kumuumiza! ndio huu ndio uongo uliopo lkn tukisimamia ukweli Usaliti nimkubwa miongoni mwetu sasa kuna haja gani yakumuamini uliye nae wakati wewe mwenyewe ni shahidi wanafsi yako kuwa unapiga matek two mengi kwa siri!.

nasema hivii…Hakuna kuaminiana kama vipi!.

kwa mfano mawasiliano yangekuwa kama yafuatayo duniani labda pengine ningefuta kauli yangu hii ya USIMUAMINI.

“mpenzi wangu wakati umesafiri nimekusaliti mara 4 na watu tofauti tofauti na mwisho wakukusaliti nj jana usiku nilitoka na best ako, so plz baby kabla hatujamet naomba tusubiri kwanza tukacheki afya! nisamehe sana mpenzi wangu kwa ukweli huu!!!”

labda haya yangekuwa ni maneno yakawaida kwa wapenzi ningeshawishika kukwambia MUAMINI lakini huo ndio ukweli unaofichwa na UONGO unaowekwa wazi ni huu

“Sijapata siku nyingi sana mpenzi yaani tangu ulivyosafiri nimevumilia, nafurahi umerudi naamini leo nitaburudika nawe, nakupenda sana”

AFANALEKI!!! Kuna haja gani yakuaminiana, eti???? usimuamini aisee!

hio ndio hali ya mambo duniani ilivyo na nitaendelea kupata dhambi kukufahamisha kitu ambacho unachokijua, kwa sasa acha nikwambie chakufanya, nalikaribia sikio lako nakunong’oneza kimbea…… USIMUAMINI!

jipende sana na uipende afya yako! kabla hujampa mwili wako mtu mtathimini kwamuda na kisha nenda ukapime nae! wakati mnaenda pia USIMUAMINI maana anaweza kumuhonga Dokta, kuwa makini.

Rudia nae kupima mara kadhaa sehemu tofauti tofauti na hata kama yuko salama usimpe kwanza mgusie suala la ndoa mradi tu aone kizuizi asikuchukulie poah! naamini ukimzungusha hivyo miezi mitatu itafika nenda mkarudie tena kupima kumbuka haya yote nikabla hujampa, ukimpa tu ujue umeshaweka rehani roho yako haikisha mnapima mara nyingi zaidi kama yuko salama ANZA SASA KUMFIKIRIA!

Sitakwambia kamwe umpe akitakacho maana mimi mwenzio imani yangu inaniambia ZINAA HAIFAI!

“usimuamini mtu ukamuudhi MUNGU wako, imani yako itakuponza, nakusihi sana ndugu yangu USIMUAMINI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

mersin escort yeni