• AUDIO
  • VIDEOS
  • ALBUM / EP
  • Dj Mix
  • E NEWS
  • Gospel
  • NIGERIA
  • Zilipendwa
Facebook Twitter Instagram
NYIMBO MPYA 2022
  • AUDIO
  • VIDEOS
  • ALBUM / EP
  • Dj Mix
  • E NEWS
  • Gospel
  • NIGERIA
  • Zilipendwa
NYIMBO MPYA 2022
You are at:Home » XXLTZ MEDIA | NYIMBO MPYA 2022 » Hadithi » Hadithi ya mapenzi iliyoshangaza dunia – Lucy na Seretse Khama ( MAKALA )
VIDEOS

Hadithi ya mapenzi iliyoshangaza dunia – Lucy na Seretse Khama ( MAKALA )

Dj StarBoyBy Dj StarBoyNovember 18, 2018No Comments2 Mins Read
Facebook Twitter Pinterest Telegram WhatsApp

Hadithi ya mapenzi iliyoshangaza dunia – Lucy na Seretse Khama ( MAKALA )

Wakati mwanamfalme wa Kiafrika na karani mmoja mwanamwali Mzungu wa maisha ya wastani kutoka kwa wamiliki wa bima wa Lloyd, walipoamua kuoana mnamo mwaka 1948, ilichochea hisia mbalimbali nchini Uingereza na Afrika.

Seretse Khama alikutana na Ruth Williams alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Oxford na wakaanza kuchumbiana.

Baada ya masomo yake, alitarajiwa kwenda nyumbani hadi katika taifa lake lililokuwa koloni ya Uingereza wakati huo ikijulikana kama Bechuanaland ambayo sasa ni Botswana, na kuoa mmoja wa watu wa kabila lake, lakini mapenzi yake kwa Williams ya libadilisha kila kitu.

Familia yake ilipinga ndoa hiyo na Khama akalazimika kukatalia mbali fursa ya kuwa mfalme.

Serikali ya Uingereza iliingilia kati na kujaribu kupinga ndoa hiyo haua iliyomfanya Khama kufukuzwa kutoka nchi yake.

Askofu wa London, William Wand, angeruhusu tu harusi inayofanyika kanisani ikiwa tu utawala nchini Uingereza ungeruhusu ndoa hiyo kufanyika. Hilo halikufanyika.

Wapenzi hao wawili walilazimika kuoana baadaye katika ofisi ya mwanasheria mkuu iliyoko Kensington huko London mnamo Septemba mwaka 1948.

Waziri mkuu wa Afrika Kusini wakati huo Daniel Malan, alitaja ndoa yao kama “iliyojaa kichefuchefu” huku mwanafunzi mmoja aitwaye Julius Nyerere, ambaye baadaye alikuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, akasema “ni mojawepo ya hadithi nzuri sana za mapenzi duniani”,

Mmoja wa walioshuhudia alizungumza na dadake Ruth Williams, ambaye alisema harusi hiyo ilikuwa “mapenzi yaliyoshinda chuki”.

Wawili hao walipata uungwaji mkubwa huku maandamano yakizidi huko Bechuanaland, kushinikiza kutambuliwa kwa ndoa hiyo ambapo baadaye walikubaliwa kurejea nchini humo mnamo mwaka 1956 baada ya watu wa kabila la Bamangwato, lake Bw Khama, walipoamua kutuma barua kwa njia ya telegram hadi kwa Malkia Elizabeth wa II.

Kufanikisha uhuru
Seretse Khama aliamua kukatalia mbali utawala wa kabila lake na akaamua kuwa mkulima na mfugaji huko Serowe. Baadaye alikibuni chama cha Bechuanaland Democratic Party na akashinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 1965.

Akiwa Waziri mkuu wa Bechuanaland (Botswana) alifanikisha nchi hiyo kujipatia uhuru mwaka 1966 na akawa Rais wa kwanza wa Botswana.

Ruth Williams Khama, alifahamika kama Lady Khama baada ya uhuru na alihudumu kama mkewe Rais wa Botswana kuanzia mwaka 1966 hadi 1980.

Walijaliwa watoto wanne: Wa kwanza Jacqueline aliyezaliwa Bechuanaland mwaka 1950; Ian aliyezaliwa England mwaka 1953, na pacha Anthony na Tshekedi waliozaliwa Bechuanaland waliozaliwa 1958.

Ian Khama ndiye Rais wa sasa wa Botswana na alianza kuongoza mwaka 2008.

Ian na Tshekedi ni wanasiasa nchini humo.

Hadithi
Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram WhatsApp
Dj StarBoy
  • Website
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram

Welcome to XXLTZ MEDIA, the number one Pure All Music platform to make your day enjoyable by making God the first choice ever everyday you work up.We publish unnumbered all Music from Africa and from Outside East Africa, but also if you wish to preach with us through your All Music , then do not hesitate to contact us and your music will be here Www.Xxltz.Xyz

YOU MAY ALSO LIKE

Jinsi ya kutumia sekunde tatu kumtongoza mwanamke ( MAKALA )

Mwanamke ukiwa na tabia hizi 7, lazima mwanaume akukimbie ( MAKALA )

Mahaba ya mwalimu – Hadithi fupi ya kusisimua mwili wako ( MAKALA )

Njia 8 zitakazo kuonesha kwamba mwanamke uliye naye atakusaidia kuleta mafanikio katika ndoa yako

Mambo 6 yatakayomfanya mumeo akupende zaidi – Ladies ( MAKALA )

Historia fupi ya maisha ya Alikiba [ MAKALA ]

Leave A Reply

Zuchu – Fire Remix
https://www.youtube.com/watch?v=QtcmQR4K3W4
JIUNGE NASI WHATSAPP
FOLLOW US
  • Facebook
  • Instagram
  • YouTube
  • Telegram
  • WhatsApp
LATEST UPDATES
AUDIO
August 13, 20220

AUDIO | Zuchu Ft Dj Starboy – Fire Remix | Download

AUDIO | Zuchu Ft Dj Starboy – Fire Remix | Download Download Audio

August 13, 2022

AUDIO | Cheed – Bado | Download

August 13, 2022

AUDIO | Cheed – Roho Yangu | Download

August 13, 2022

AUDIO | Cheed Ft Anjella – Umenikatili | Download

August 13, 2022

AUDIO | Cheed – Kisu | Download

August 13, 2022

AUDIO | Karole Kasita Ft Eddy Kenzo – Tubiddemu | Download

August 13, 2022

AUDIO | Galatone Ft Stamina – Utakubali | Download

August 12, 2022

AUDIO | Rayvanny – Azam | Download

August 12, 2022

AUDIO | Meja Kunta – Asie Cheat Nani | Download

August 12, 2022

AUDIO | Martha Mwaipaja – ADUI | Download

COMEDY😂🤣 KALI YA LEO
https://www.youtube.com/watch?v=uVFsxG3gIbU&t=15s
NOW TRENDING
AUDIO
August 13, 20220

AUDIO | Zuchu Ft Dj Starboy – Fire Remix | Download

AUDIO | Zuchu Ft Dj Starboy – Fire Remix | Download Download Audio

August 12, 2022

AUDIO | CHEED Ft. HARMONIZE – Konkodi | Download

August 12, 2022

AUDIO | CHEED Ft. Anjella – Chombo | Download

August 11, 2022

AUDIO | Rayvanny – ODG Remix Ft. Eltee Skhillz | Download

August 10, 2022

AUDIO | Country Wizzy Ft. Marioo – Poa | Download

August 6, 2022

Nymbo Mpya Za NANDY 2022

August 6, 2022

AUDIO | Nandy Ft. Dulla Makabilla – Hatujui | Download

August 6, 2022

AUDIO | Nandy Ft. Lody – Unanimaliza | Download

August 6, 2022

AUDIO | D voice – Nawaza Siku Nikifa | Download

August 6, 2022

AUDIO | Lody music X Msami kizzy – ASANTE | Download

August 4, 2022

AUDIO | Ibraah – Tusamehe | Download

August 1, 2022

VIDEO | Zuchu – Fire | Download

July 29, 2022

AUDIO | Harmonize – Miss Bantu Ft. Spice | Download

July 28, 2022

VIDEO | Lava Lava – Desh Desh | Download

July 26, 2022

AUDIO | Ronze Ft. LodyMusic – Naanzaje | Download

July 26, 2022

AUDIO | Nacha – Ruksa | Download

July 26, 2022

VIDEO | Nacha – Ruksa | Download

Copyright © 2022 XXLTZ MEDIA. By Dj StarBoy.
  • PROMOTE YOUR MUSIC
  • ALBUM / EP
  • AUDIO
  • VIDEOS
  • Bongo Kitambo tbt
  • Singeli
  • WCB WASAFI
  • USA SONG
  • Beat Za Injili
  • HIP HOP Music
  • KASWIDA
  • Netflix
  • MOVIES
  • SoundCloud
  • Privacy Policy
  • Amazon
  • Contact Us
  • About US

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.