Browse

Categories

Company

Nay wa Mitego ni sawa na Gigy Money na Amber Lulu! – Dudu Baya

Posted On: July 8, 2017 By NYIMBO MPYA 2024
Stream and Download Nyimbo Mpya 2024 Bongo Fleva Mpya 2024 latest new Songs released 2024 from your favorite Artists and enjoy Mp3 Music Audio and HD New Song Videos of different Styles such as Bongo flava, Hip Hop, Afrobeats, Kwaito, House, Amapiano, Gospel, Zouk/Rhumba & More.

Download Nyimbo Mpya

PLAY
SHARE
   19

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Dudu Baya amedai muziki wa rapa Nay wa Mitego hautofautiani sana na muziki wa Gigy Money na Amber Lulu huku akidai ni muziki uliotawaliwa na majungu na majigambo
.

Akiongea na Najma Media Ijumaa hii, Dudu amewashangaa mashabiki wa muziki kuendelea kumpatia support rapa huyo wakati haoni chochote anachofanya kwenye muziki.
“Mimi sio shabiki wa muziki wa Nay wa Mitego, kwanza muziki wake haueleweki ndio maana namfananisha na Amber Lulu na Gigy Money,” alisema Dudu Baya. “Kuna wasanii wakali wanafanya muziki mzuri kuliko huyo lakini hawapewi support, mimi ningewashauri tu mashabiki wa muziki wapende muziki mzuri,”
Alisema hajui rapa huyo anafanya muziki wa namna gani kwani amekuwa ni msanii wa hip hop anayetumia mwamvuli wa hip hip kuwasema watu.
Rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki kusikiliza muziki mzuri ambao utawajenga na sio muziki ambao ndani yake una maneno ya kuwasema watu bila sababu.

More from Nay wa

VIDEO | Nay Wa Mitego – Bachela   
Posted On:  April 30, 2024
AUDIO | Nay Wa Mitego – Bachela   
Posted On:  April 14, 2024

Featured Artists  View All