Baraka The Prince ana akili za kitoto – Alikiba

Muimbaji Alikiba ambaye hivi karibuni ametangazwa na RockStar4000 kuwa mmoja kati ya wamiliki wa label hiyo, amefunguka kwa kudai kuwa msanii wa label hiyo, Baraka The Prince ana akili za kitoto ndio maana kuna maadhi ya mambo yanaibuka kwamba haelewani na baadhi ya wasanii wenzake.


Hit maker huyo wa Aje amesema hayo baada ya kuulizwa kwamba kwa sasa hawaonekani kuwa karibu na Baraka kama zamani huku tetesi zikidai kwamba ukaribu wao umevunjika baada ya Alikiba kuwa karibu na Ommy Dimpoz.
“Mimi nadhani ni utoto tu, nadhani ni umri tu lakini Baraka yupo vizuri, ni mtu anayesikiliza na ana rekebishika. Muda mwingine labda umri ndio unampeleka lakini muda mwingine mtoto akifanya jambo unamwambia,” Alikiba alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM. “Ni mdogo wetu tutamwelimisha na sidhani kama anamchukia Ommy Dimpoz labda ni maneno tu ya mtaani,”
Kwa upande wa Ommy Dimpoz ambaye alitambulisha wimbo wake mpya Cheche, amedai yeye hajawahi kugombana na Baraka na wala hana tatizo na mtu yeyote.
Muimbaji hapo jana amesainiwa mkataba na label ya RockStar4000 na kuungana na Baraka The Prince pamoja na Lady Jay Dee ambao wapo kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

mersin escort yeni