Amber Lulu autosa ‘u-video queen’, aingia rasmi kwenye muziki

Baada ya kufanya vizuri na wimbo Watakoma, msanii na mrembo Amber Lulu amedai hawezi tena kufanya kazi ya u-video queen ambayo imemtoa kwa madai anaona kama atakuwa anajirudisha nyuma kimuziki.

Amber huyo wa Bongo, amedai tayari ameshaona anaweza kufanya muziki na akafanikiwa zaidi na sio kuendelea kuwa video queen.
“Sasa hivi nafanya muziki sio video vixen tena kwa sababu nimeshaingia kwenye muziki kwa hiyo nikifanya video vixen nakua kama narudi nyuma na mimi sitaki kurudi nyuma tena nahitaji nifanye vitu vipya,” Amber Lulu alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Inatakiwa kama ni muziki wangu niufanye wa international au nizidishe sitaki kurudishana nyuma”
Hata hivyo Amber amesema amekuwa akipokea maoni tofauti tofauti kutokana na wimbo wa ‘Watakoma’ wengi wakitoa sifa na kumtia moyo.
“Napokea maoni mengi mazuri, mfano kuna baadhi ya wasanii kama wakina Shilole na Chege nimeshakaa nao kuna vitu wameniambia unatakiwa ufanye,” aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

mersin escort yeni