Browse

Categories

Company

Maporomoko ya ardhi yaua watoto 44 Colombia

Posted On: April 3, 2017 By NYIMBO MPYA 2024
Stream and Download Nyimbo Mpya 2024 Bongo Fleva Mpya 2024 latest new Songs released 2024 from your favorite Artists and enjoy Mp3 Music Audio and HD New Song Videos of different Styles such as Bongo flava, Hip Hop, Afrobeats, Kwaito, House, Amapiano, Gospel, Zouk/Rhumba & More.

Download Nyimbo Mpya

PLAY
SHARE
   31

_95430462_7d9f8140-ffee-4c0e-8b6f-65d320583ae5
Raia wa Colombia walionusurika kwenye ajali ya maporomoko ya ardhi katika mji ulio kusini mwa nchi hiyo Mocoa, wamekuwa wakifukua vifusi kuwatafuta watu ambao mpaka sasa hawajulikani walipo.
Asilimia 30 ya mji huo umeathiriwa na maporomoko hayo.
Watu 254 wanaelezwa kupoteza maisha kwenye tukio hilo baya siku ya ijumaa Dimitri O’ Donnell ni mwandishi wa Habari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bogota
” Katika kipindi cha saa tatu , asilimia 30 ya mvua ambayo hunyesha mjini Mocoa, kwa mwezi ilinyesha kwa saa hizo tatu, kiasi ambacho kingenyesha kwa siku takriban 10, kwa hiyo ilikua mvua ya kumshtua kila mtu”
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ambaye anautembelea mji wa Mocoa kwa siku mbili sasa amesema zaidi zaidi ya watu 200 wamebainika kupoteza maisha, miongoni mwao watoto 44. idadi zaidi ya waliopoteza maisha inatarajiwa kuongezeka kwa kuwa bado watu takriban 300 bado hawajulikani walipo.
Mwanabaiolojia Carolina Pardo kutoka chuo kikuu cha El Rosario mjini Bogota,amezungumza na BBC akisema matumizi mabaya ya ardhi yamesababisha mmomonyoko wa udongo uliosababisha maporomoko ya ardhi.

More from Maporomoko ya

Featured Artists  View All